23 Februari 2025 - 19:26
Mwanamke Mlebanoni aliyekaidi marufuku ya kuinua picha ya Nasrullah kwenye Uwanja wa Ndege wa Beirut azungumza

Asmaa Bzeih mwanamke kijana Mlebanoni mwenye umri wa miaka 27 ambaye amekuwa nembo ya upinzani baada ya hivi karibuni kukabiliana na maafisa husika katika uwanja wa ndege wa Beirut amesema kuwa dunia inapasa kuungana na Muqawama.

Bzeih aliwavutia watu wengi wiki iliyopita baada ya kukataa amri ya kiimla ya kutobeba juu picha za Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah katika Uwanja wa Ndege wa Beirut, Lebanon.

Video iliyomuonyesha Bi Asmaa akikabiliana na maafisa husika uwanjani hapo huku akiwakumbusha njama za maadui, ilisambaa katika mitandao na vyombo mbalimbali vya habari. Mwanamke huyo Mlebanoni alikumbana na amri hiyo wakati akirejea nchini baada ya kutoka katika ziara katika mji mtakatifu wa Mash'had nchini Iran.

Akizungumza na tovuti ya televisheni ya Press, Asmaa Bzeih ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, amewatolea wito walimwengu kuunga na kupinga aina zote za ukandamizaji na kuunga mkono pakubwa mapambano ya ukombozi.

Aidha amewatolea wito duniani kote kuhudhuria shughuli ya mazishi ya Shahidi Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah na Naibu wake Sayyid Hashim Safiyuddin akitilia mkazo umuhimu wa ushiriki mkubwa wa watu katika tukio hili la kihistoria.

"Adui anahofia madhuhurio makubwa ya watu, akijua kwamba mikusanyiko mikubwa kama hiyo itasambaratisha propaganda zao, itasambaratisha njama zao za kuidhibiti dunia, na njama zao mbovu dhidi ya Muqawama na wafuasi wake," amesema Asmaa Bzeih.

342/